Baada ya kuelewa maana na umuhimu wa Media Kit hatua inayofuata ni kujua ni taarifa gani zinapaswa kuwepo ndani yake.Media Kit nzuri si mkusanyiko wa maneno mengi bali ni nyaraka iliyoandaliwa kwa mpangilio mzuri yenye taarifa sahihi na rahisi kueleweka.Kampuni nyingi huchukua dakika chache tu kuipitia Media Kit.Ndiyo maana ni muhimu kuonyesha taarifa muhimu kwa njia ya kuvutia na ya kitaalamu.
1. Jina la Blog na Nembo (Logo)
Sehemu ya kwanza ya Media Kit
inapaswa kuonyesha utambulisho wa blog yako.
Weka:
i.
Jina
la blog.
ii.
Nembo
(Logo).
iii.
Kaulimbiu
(Tagline), ikiwa unayo.
Kwa mfano:
DALUSOFA Blog
"Maarifa,Teknolojia,Blockchain
na Fursa za Kipato Mtandaoni."
Utambulisho huu husaidia
kampuni kukumbuka blog yako kwa urahisi.
2. Kuhusu Blog (About the Blog)
Eleza blog yako kwa kifupi
lakini kwa kuvutia.
Jibu maswali kama:
i.
Blog
ilianzishwa lini?
ii.
Inaandika
kuhusu nini?
iii.
Dhamira
yake ni ipi?
iv.
Inawasaidiaje
wasomaji?
Mfano:
"DALUSOFA Blog ni blog inayotoa
elimu kuhusu blockchain,teknolojia, AI,Web3,biashara mtandaoni na fursa za
kuongeza kipato.Lengo letu ni kuwapa wasomaji maarifa sahihi na yanayoweza
kutumika katika maisha ya kila siku."
3. Kuhusu Mwandishi (About the Author)
Wadhamini wanataka kujua ni
nani anayesimamia blog.
Andika kwa kifupi:
i.
Jina
lako.
ii.
Uzoefu
wako.
iii.
Maeneo
unayobobea.
iv.
Dhamira
yako.
Usiandike wasifu mrefu sana.Eleza
mambo muhimu yanayojenga uaminifu.
4. Dhamira na Maono
Onyesha kusudi la blog yako.
Mfano:
Dhamira:
"Kutoa elimu sahihi kuhusu teknolojia na fursa za kidijitali kwa lugha
rahisi ya Kiswahili."
Maono:
"Kuwa moja ya blog zinazoongoza Afrika Mashariki katika elimu ya
blockchain,AI na biashara mtandaoni."
Dhamira na maono vinaonyesha
kuwa blog yako ina mwelekeo wa muda mrefu.
5. Aina ya Wasomaji (Audience)
Hiki ni moja ya vipengele
muhimu zaidi.
Eleza watu wanaosoma blog yako.
Mfano:
· Vijana.
· Wanafunzi.
· Wafanyabiashara.
· Wafanyakazi.
· Wadau wa teknolojia.
· Wapenzi wa blockchain.
· Wanaotafuta njia za kupata kipato
mtandaoni.
Kadri unavyowafahamu wasomaji
wako ndivyo wadhamini watakavyoona thamani ya blog yako.
6. Takwimu za Blog
Kampuni nyingi hupenda kuona
takwimu halisi.
Unaweza kuonyesha:
· Idadi ya wageni kwa mwezi.
· Kurasa zinazotazamwa.
· Nchi ambazo wageni wanatoka.
· Ukuaji wa blog.
Ikiwa bado unaanza na takwimu
ni ndogo,usidanganye.Weka taarifa za kweli na uendelee kuzisasisha kadri blog
inavyokua.
7. Mitandao ya Kijamii
Onyesha majukwaa yote unayotumia.
Kwa mfano:
· Facebook.
· YouTube.
· TikTok.
· Instagram.
· X.
· Telegram.
Kampuni nyingi huangalia pia
ushawishi wako nje ya blog.
8. Huduma Unazotoa
Eleza wazi huduma ambazo
kampuni zinaweza kupata kupitia wewe.
Mfano:
· Sponsored Posts.
· Product Reviews.
· Banner Advertising.
· Affiliate Marketing.
· Guest Posts.
· Social Media Promotion.
Kadri huduma zinavyowekwa wazi
ndivyo wadhamini wanavyoweza kufanya maamuzi kwa urahisi.
9. Kampuni Ulizowahi Kushirikiana Nazo
Ikiwa umewahi kufanya kazi na
kampuni yoyote itaje.
Mfano:
· Kampuni za teknolojia.
· Mashirika.
· Biashara ndogo.
· Miradi ya kijamii.
Hata kama ni ushirikiano mdogo
unaweza kuutaja ikiwa ulikuwa wa mafanikio.
10. Ushuhuda (Testimonials)
Maoni ya watu waliowahi kufanya
kazi na wewe yanaongeza uaminifu.
Mfano:
"DALUSOFA Blog ilitusaidia
kuwafikia wasomaji wengi waliovutiwa na huduma zetu.Ushirikiano ulikuwa wa
kitaalamu na wenye matokeo mazuri."Ushuhuda mfupi unaweza kuwa na nguvu
kubwa katika kuwashawishi wadhamini.
11. Mawasiliano
Media Kit isikose sehemu ya
mawasiliano.
Weka:
· Barua pepe.
· Namba ya simu (ikiwa unataka).
· Kiungo cha blog.
· Viungo vya mitandao ya kijamii.
Mawasiliano yawe rahisi
kupatikana ili mdhamini aweze kuwasiliana nawe haraka.
Hitimisho
Media Kit yenye taarifa hizi
inaonyesha kuwa blog yako imeandaliwa kwa kiwango cha kitaalamu.Hata kama bado
unaanza,kuwa na Media Kit iliyoandikwa vizuri kunaweza kukutofautisha na
bloggers wengi ambao hawana nyaraka hii.Katika Sehemu inayofuata,tutajifunza
jinsi ya kubuni (design) Media Kit yenye muonekano wa kuvutia,jinsi ya kutumia Canva
au zana nyingine za bure na mbinu za kuifanya ionekane ya kisasa na ya
kitaalamu ili kuvutia wadhamini.
No comments:
Post a Comment