Makosa Makubwa ya Kuepuka Unapotumia 2FA
Kosa la Kwanza: Kutoa OTP
OTP ni code ya muda
mfupi.Hata kama mtu anasema:“Mimi ni support.”Usitoe code bila kuthibitisha.Mtu
wa kweli wa support kwa kawaida hahitaji password yako au code yako ya siri ili
“kukusaidia” kwa njia ya ujumbe wa kawaida.
Kosa la Pili: Kushiriki Recovery Codes
Recovery codes zinaweza
kutumika kurejesha ufikiaji wa akaunti.Zihifadhi mahali salama.Usizitume
kwenye:
- WhatsApp
- Facebook messages
- Email zisizo salama
Kosa la tatu:Kutumia Password Moja
2FA ni nzuri lakini
password tofauti bado ni muhimu.
Kukubali Push Notification Bila Kuangalia
Kabla ya kubonyeza
“Approve”, jiulize:Je, mimi ndiye niliyejaribu kuingia?Kama si wewe, kataa.
Kosa la Tano: Kutokuwa na Backup
Unaweza kupoteza:
- Simu
- Authenticator app
- Security key
Kuwa na njia ya recovery.
Jinsi ya Kuwasha 2FA
Ingawa kila huduma ina
muonekano tofauti, hatua za kawaida ni:
1.
Ingia kwenye akaunti yako.
2.
Fungua Settings.
3.
Tafuta Security.
4.
Tafuta Two-Factor
Authentication au 2-Step Verification.
5.
Chagua njia ya 2FA.
6.
Fuata maelekezo.
7.
Hifadhi recovery codes.
Kwa kawaida unaweza kuona
majina kama:
- Two-Factor Authentication
- 2FA
- 2-Step Verification
- Multi-Factor Authentication
No comments:
Post a Comment