Baada ya kuelewa maana ya
Blockchain na historia yake,swali linalofuata ni:Blockchain inafanyaje
kazi?Ingawa teknolojia hii inaweza kuonekana ngumu mwanzoni,msingi
wake ni rahisi kuelewa ukiufuata hatua kwa hatua.Fikiria una daftari ambalo
watu wengi duniani wana nakala yake.Kila unapoongeza taarifa mpya kwenye
daftari hilo,kila mtu hupata nakala hiyo mpya.Hakuna mtu anayeweza kubadilisha
taarifa kwa siri bila wengine kugundua.Huo ndio msingi wa Blockchain.
Hatua ya 1:Muamala Unaombwa
Kila kitu huanza pale mtu
anapotaka kufanya muamala.
Mfano:
· Kutuma Bitcoin kwa rafiki.
· Kununua NFT.
· Kutuma tokeni.
· Kutekeleza Smart Contract.
Mfumo hupokea ombi hilo na
kuanza kulichunguza.
Hatua ya 2: Muamala Unatangazwa Kwenye Mtandao
Baada ya ombi kutumwa taarifa
hiyo husambazwa kwenye mtandao wa Blockchain.Mtandao huu una maelfu ya kompyuta
zinazoitwa Nodes.
Node ni Nini?
Node ni kompyuta
iliyounganishwa kwenye mtandao wa Blockchain.
Kazi za node ni pamoja na:
· Kupokea miamala mipya.
· Kuhifadhi nakala ya Blockchain.
· Kuthibitisha miamala.
· Kushiriki taarifa na node nyingine.
Kadri idadi ya nodes
inavyoongezeka ndivyo mtandao unavyokuwa salama zaidi.
Hatua ya 3:Muamala Unathibitishwa
Nodes hukagua kama muamala ni
halali.Huangalia mambo kama:
· Je,mtumaji ana salio la kutosha?
· Je,sahihi ya kidijitali (Digital
Signature) ni sahihi?
· Je,sheria za mtandao zimefuatwa?
Kama kila kitu kiko sawa
muamala unaruhusiwa kuendelea.
Hatua ya 4:Muamala Unawekwa Ndani ya Block
Baada ya kuthibitishwa muamala
huunganishwa na miamala mingine ndani ya Block.
Block ni Nini?
Block ni kifurushi cha taarifa.
Ndani yake kuna:
· Orodha ya miamala.
· Muda wa kutengenezwa.
· Hash ya block.
· Hash ya block iliyotangulia.
Kwa sababu kila block
inaunganishwa na iliyotangulia hutengeneza mnyororo unaoitwa Blockchain.
Hash ni Nini?
Hash ni msimbo wa kipekee
unaotengenezwa kutokana na taarifa zilizopo ndani ya block.Unaweza kuufikiria
kama alama ya kidole/finger print.Kama taarifa ndani ya block zitabadilishwa
hata kwa herufi moja tu:
· Hash hubadilika kabisa.
· Mtandao hugundua kuwa kuna tatizo.
· Block hiyo hukataliwa.
Ndiyo maana Blockchain ni
vigumu kuchezewa.
Hatua ya 5:Consensus
Baada ya block kutengenezwa
mtandao lazima ukubaliane kuwa ni halali.Mchakato huu huitwa Consensus.Consensus
ni mfumo unaofanya kompyuta nyingi zikubaliane kuhusu taarifa sahihi.Bila
Consensus kila mtu angeweza kuandika taarifa anazotaka.
i.
Proof of Work (PoW)
Mfumo huu hutumiwa na Bitcoin.
Kompyuta maalumu hushindana
kutatua tatizo la kihesabu.Anayefaulu kwanza:
· Huthibitisha block.
· Hupata zawadi ya Bitcoin.
Faida:
Usalama
mkubwa.
Changamoto:
Hutumia
umeme mwingi.
ii.
Proof of Stake (PoS)
Mfumo huu hutumiwa na mitandao
mingi ya kisasa kama Ethereum.Badala ya kutumia nguvu kubwa za kompyuta
uthibitishaji hufanywa na watu walioweka (stake) sarafu zao kama dhamana.
Faida zake:
· Matumizi madogo ya umeme.
· Kasi kubwa ya miamala.
· Gharama ndogo.
Hatua ya 6: Block Inaongezwa Kwenye Blockchain
Baada ya kukubaliwa na mtandao:
· Block huongezwa kwenye Blockchain.
· Nakala mpya husambazwa kwa nodes zote.
· Rekodi huwa sehemu ya historia ya
kudumu.
Hapo muamala unakuwa
umekamilika.
Kwa Nini Ni Vigumu Kubadilisha Blockchain?
Kila block:
· Ina hash yake.
· Ina hash ya block iliyotangulia.
Ukibadilisha taarifa kwenye
block moja:
· Hash hubadilika.
· Block zinazofuata hazitalingana.
· Nodes nyingine zitakataa mabadiliko
hayo.
Ili kufanikiwa kubadilisha
Blockchain mtu angehitaji kudhibiti sehemu kubwa ya mtandao kwa wakati mmoja
jambo ambalo ni gumu sana kwenye mitandao mikubwa.
Mfano Rahisi wa Blockchain
Fikiria una vitabu 100 vya
kumbukumbu.Kila mtu kwenye kijiji ana nakala yake.Ukiandika taarifa mpya au kwa
mfano rahisi zaidi,wewe umetengeneza kundi/groups za whatsapp na watu
wakajiunga kwenye group lako,maana yake kila meseji utakayotuma watu wote
waliopo kwenye group lako:
· Wote hupata nakala mpya.
· Mtu mmoja akifuta taarifa kwenye kitabu
chake,wengine bado wana nakala sahihi.
· Jamii nzima inaweza kuthibitisha kitabu
gani ni sahihi.
Hivyo ndivyo Blockchain
inavyolinda taarifa.
Faida za Mfumo Huu
Kwa kutumia mfumo huu:
· Hakuna benki au kampuni moja
inayodhibiti taarifa.
· Rekodi haziwezi kubadilishwa kirahisi.
· Watu wanaweza kuaminiana hata bila
kufahamiana.
· Miamala inaweza kufanyika kwa uwazi
zaidi.
Hitimisho
Blockchain hufanya kazi kwa
kuunganisha kompyuta nyingi katika mtandao unaoshirikiana kuthibitisha na
kuhifadhi taarifa kwa usalama.Kuanzia muamala unaotumwa,kuthibitishwa,kuwekwa
ndani ya block na hatimaye kuongezwa kwenye Blockchain.Kila hatua inalenga
kuhakikisha taarifa ni sahihi na haziwezi kubadilishwa bila idhini ya mtandao.Katika
Sehemu inayofuata tutajifunza vipengele muhimu vya
Blockchain,ikiwa ni pamoja na Decentralization,Transparency,Immutability,Cryptography,Smart
Contracts na Security na kwa nini vinaifanya Blockchain kuwa
teknolojia ya kipekee.
No comments:
Post a Comment