Akaunti Gani Zinapaswa Kuwa na 2FA?
Kama huwezi kuwasha 2FA
kila mahali mara moja, anza na akaunti muhimu.
1. Email
Email ni muhimu sana kwa
sababu inaweza kutumika kurejesha passwords za akaunti nyingine.
2. Benki na huduma za fedha
Linda akaunti
zinazohusiana na fedha.
3. Social Media
Facebook, Instagram,
TikTok na nyingine zinaweza kutumiwa kuwasiliana na watu wengi.Akaunti
ikichukuliwa, wahalifu wanaweza kutumia jina lako kufanya utapeli.
4. Cloud Storage
Documents muhimu zinaweza kuwepo
huko.
5. Cryptocurrency
Wallets na exchanges
zinaweza kuhusisha fedha.Kwa hiyo ulinzi wa ziada ni muhimu.
Kwa Nini Email Inapaswa Kulindwa Kwanza?
Email ni kama kitovu cha
akaunti nyingi.Ukisahau password ya:
- Facebook
- Instagram
- Website
- Shopping account
Mara nyingi utapewa link
ya kurejesha kupitia email.Kwa hiyo, mtu akipata email yako, anaweza kujaribu
kurejesha akaunti nyingine.Ndiyo maana:Linda email yako kwa password imara
na 2FA.
2FA na Social Media
Akaunti za social media
zinaweza kuwa na:
- Wafuasi
- Ujumbe binafsi
- Biashara
- Matangazo
- Pages
Akaunti ikichukuliwa
inaweza kutumiwa:
- Kutuma scams
- Kuomba fedha
- Kutuma links hatari
- Kuharibu sifa
2FA inaweza kupunguza
hatari ya mtu kutumia password yako pekee kuingia.Lakini bado kuwa makini na
phishing.
No comments:
Post a Comment