Monday, October 26, 2026

Kwa Nini Baadhi ya Wachungaji Wanasema AI ni Mpinga Kristo?


Katika miaka ya hivi karibuni, Artificial Intelligence, maarufu kama AI, imeingia kwa kasi katika maisha ya watu. Leo tunaona AI ikitumika kwenye simu, kompyuta, biashara, elimu, utafiti, mawasiliano na hata katika huduma za Kanisa.Lakini pamoja na maendeleo hayo, kuna jambo ambalo limezua mjadala mkubwa miongoni mwa Wakristo.Baadhi ya wachungaji na wahubiri wamekuwa wakisema kwamba AI inaweza kuwa sehemu ya mfumo wa Mpinga Kristo, na wengine wamefikia kusema moja kwa moja kwamba AI ni Mpinga Kristo.

Kauli hii imewafanya Wakristo wengi kujiuliza:

Je, AI kweli ni Mpinga Kristo?

Biblia inasema nini kuhusu jambo hili?

Kwa nini baadhi ya wachungaji wanaunganisha AI na Mpinga Kristo?

Na muhimu zaidi, tunapaswa kuamini nini kama Wakristo?

Makala hii haikusudii kumhukumu mchungaji yeyote wala kusema kwamba hofu zote kuhusu AI hazina msingi. Badala yake, tunataka kuchunguza kwa utulivu sababu zinazofanya baadhi ya viongozi wa Kikristo kufikia hitimisho hilo, na pia kuangalia kile Biblia inachosema kuhusu Mpinga Kristo.

AI ni nini?

Kabla hatujaingia kwenye suala la Mpinga Kristo, ni muhimu kwanza kuelewa AI ni nini.AI ni teknolojia inayowezesha mifumo ya kompyuta kufanya kazi ambazo kwa kawaida zinahitaji uwezo fulani wa kibinadamu, kama kuchanganua taarifa, kutafsiri lugha, kutengeneza maandishi, kutambua mifumo na kusaidia katika kutatua matatizo.Kwa sababu AI inaweza kuzungumza na kutoa majibu kwa namna inayofanana na mwanadamu, watu wengine wameanza kuiangalia kama kitu kinachoweza kuwa na uwezo wa kipekee sana.Na hapa ndipo hofu inaanza.Mtu anaweza kujiuliza:“Ikiwa mashine inaweza kufikiri na kuzungumza kama mwanadamu, je, siku moja inaweza kutawala mwanadamu?”Swali hili si la Wakristo pekee. Ni mjadala unaohusu jamii nzima.

Mpinga Kristo ni nani?

Kabla ya kusema AI ni Mpinga Kristo, tunahitaji kwanza kuelewa neno “Mpinga Kristo” linamaanisha nini katika Biblia.

Neno hili linatajwa hasa katika nyaraka za Yohana.Biblia inasema:“Watoto wadogo, ni wakati wa mwisho; na kama mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo...” 1 Yohana 2:18

Pia tunasoma:

“Ni nani aliye mwongo ila yeye akanaye ya kuwa Yesu ni Kristo? Huyo ndiye mpinga Kristo...”  1 Yohana 2:22

Na katika 1 Yohana 4:3 tunaona pia wazo la roho ya mpinga Kristo.Hii inatupa jambo muhimu la kuzingatia.

Biblia inapozungumza kuhusu mpinga Kristo, inazungumzia zaidi ya teknolojia. Inahusisha upinzani dhidi ya Kristo na ukweli wa Injili.Kwa hiyo, kusema tu kwamba:

“AI inaweza kuzungumza, kwa hiyo AI ni Mpinga Kristo”

hakutoshi kuthibitisha jambo hilo kibiblia.

Kwa hiyo, tunapaswa kuogopa AI?


Nadhani swali hili linahitaji jibu lenye usawa.Hatupaswi kuishi kwa hofu isiyo na msingi.

Lakini pia hatupaswi kuwa wajinga kuhusu hatari zinazoweza kuletwa na teknolojia.AI inaweza kutusaidia.AI inaweza pia kutumiwa vibaya.Kwa hiyo, tunahitaji maarifa na tahadhari kwa pamoja.Kama Wakristo, tunapaswa kujifunza teknolojia bila kuiacha ichukue nafasi ya Mungu katika maisha yetu.Tunapaswa kutumia AI bila kupoteza uwezo wetu wa kufikiri.Tunapaswa kutumia AI bila kuacha ukweli.Na tunapaswa kutumia teknolojia bila kupoteza utu wetu.

Hitimisho

AI imekuja na itazidi kuwa sehemu ya maisha yetu.Tunaweza kuikataa, kuiogopa au kujifunza namna ya kuitumia.

Lakini jambo moja ni wazi: tunahitaji kuwa na ufahamu wa teknolojia tunayoishi nayo.Kwa Mkristo, suala si tu kama AI ni nzuri au mbaya.Swali kubwa ni:

“Nitaitumiaje?”

Je, nitatumia AI kujifunza?

Je, nitatumia kusaidia wengine?

Je, nitatumia katika kazi yangu?

Je, nitatumia katika huduma?

Au nitaanza kuitegemea mpaka nisifikirie mwenyewe?

Hapo ndipo uchaguzi wetu unapokuwa muhimu.

Biblia inasema:

“Jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema.”  1 Wathesalonike 5:21

Kwa hiyo, tusiiogope AI kwa sababu tu ni mpya.

Tusiiamini kupita kiasi kwa sababu tu ina uwezo mkubwa.

Tujifunze. Tuchunguze. Tuitumie kwa hekima.

Na zaidi ya yote, tukumbuke kwamba teknolojia inaweza kubadilika kila siku, lakini nafasi ya Mungu katika maisha ya mwanadamu haiwezi kuchukuliwa na mashine.

AI inaweza kutusaidia kupata taarifa, lakini hekima ya kweli bado inahitaji mwanadamu mwenye utambuzi, maadili na kumcha Mungu.

Wewe unaonaje AI?

Je, unaamini AI ni fursa kwa Kanisa, ni tishio, au ni teknolojia ambayo inaweza kuwa na manufaa na madhara kulingana na namna tunavyoitumia?

Tuambie maoni yako kwenye sehemu ya maoni.

Monday, October 19, 2026

Je, AI inaweza kutufanya tuwe wavivu?


Ndiyo, hili ni jambo tunalopaswa kulifikiria.

Fikiria mwanafunzi ambaye kila anapopewa kazi anaenda moja kwa moja kwa AI na kunakili jibu.

Anaweza kupata kazi nzuri, lakini je, amejifunza?

Au fikiria mtu ambaye hataki tena kusoma kwa sababu anaweza kuuliza AI kila kitu.

Hapo kuna tatizo.

Teknolojia inapaswa kutusaidia kufikiri, si kutufanya tuache kufikiri.

Kama AI inakusaidia kuelewa jambo, ni vizuri.

Lakini kama AI imefanya usome kidogo, ufikiri kidogo na ujifunze kidogo, basi matumizi yako yanahitaji kurekebishwa.

 

Kanisa lisiiogope teknolojia bila kuielewa

Ninaamini Kanisa linahitaji kuwa sehemu ya mazungumzo haya.

Hatupaswi kuwa watu wanaokataa kila kitu kipya.

Lakini pia hatupaswi kuwa watu wanaokubali kila kitu kipya bila kuchunguza.

Tunapaswa kuwa katikati:

kujifunza, kuchunguza na kutumia kwa hekima.

Vijana wetu tayari wanaishi katika dunia ya teknolojia.

Kwa hiyo, ni bora Kanisa liwafundishe namna ya kutumia teknolojia kwa uadilifu kuliko kuwaacha wajifunze kila kitu kutoka sehemu ambazo hazina msingi mzuri.

 

Tunahitaji hekima kuliko teknolojia

AI inaweza kutupa taarifa nyingi sana.

Lakini taarifa nyingi si sawa na hekima.

Unaweza kuwa na taarifa nyingi na bado ukafanya uamuzi mbaya.

Ndiyo maana Biblia inasema:

“Kumcha BWANA ni mwanzo wa hekima.” — Mithali 9:10

Katika kizazi hiki, tunahitaji watu wanaojua teknolojia, lakini pia tunahitaji watu wenye tabia njema, ukweli, hekima na uwajibikaji.

AI inaweza kuwa na uwezo mkubwa, lakini bado mwanadamu ndiye anayewajibika kwa namna anavyotumia uwezo huo.

Wednesday, October 7, 2026

AI inaweza kusaidia katika kazi ya Kanisa


Hapa ndipo ninapoona kuna jambo ambalo Wakristo wanapaswa kulifikiria kwa makini.

AI inaweza kutumika kusaidia katika huduma mbalimbali.

Mchungaji anaweza kuitumia kupata mawazo ya utafiti.

Mwalimu wa Biblia anaweza kuitumia kuandaa maswali ya wanafunzi.

Mtu anayefanya kazi ya kutafsiri anaweza kuitumia kama msaada wa awali.

Kanisa linaweza kutumia teknolojia kusaidia kuandaa maudhui ya elimu, video, matangazo na machapisho ya mitandao ya kijamii.

Lakini kuna tofauti kubwa kati ya kutumia AI kama chombo na kuifanya AI kuwa chanzo cha imani.

Hapo ndipo tunapaswa kuweka mpaka.

AI haiwezi kuchukua nafasi ya Mungu

Hili ndilo jambo ambalo Mkristo hapaswi kulisahau.

AI inaweza kukusaidia kutafuta taarifa kuhusu Biblia.

Lakini AI si Mungu.

AI inaweza kukusaidia kuandaa somo.

Lakini AI si Roho Mtakatifu.

AI inaweza kukusaidia kupanga mawazo ya mahubiri.

Lakini AI haiwezi kuchukua nafasi ya maisha yako ya maombi na uhusiano wako na Mungu.

Hii ni muhimu sana kwa sababu kuna hatari ya mwanadamu kuanza kutegemea teknolojia kupita kiasi.

Tunapaswa kutumia teknolojia, lakini tusiruhusu teknolojia itumie sisi.

Tatizo jingine: AI inaweza kukosea

Wakati mwingine watu wanapopata jibu kutoka kwa AI wanafikiri lazima liwe sahihi.

Lakini si lazima.

AI inaweza kutoa jibu ambalo linaonekana zuri lakini likawa na makosa.

Inaweza kuchanganya taarifa.

Inaweza kutoa rejea isiyo sahihi.

Inaweza hata kueleza jambo la Biblia kwa namna ambayo haikubaliki na muktadha wa maandiko.

Kwa hiyo, hasa katika mambo ya imani, usichukue kila jibu la AI kama ukweli wa mwisho.

Soma Biblia.

Chunguza muktadha.

Tafuta vyanzo vinavyoaminika.

Uliza watu wenye ujuzi.

Na zaidi ya yote, tumia hekima.

Kwa Nini Wakristo na Watu Wengine Wanaogopa AI?

 

Katika miaka ya hivi karibuni, kuna teknolojia moja ambayo imekuwa ikizungumziwa sana duniani: Artificial Intelligence au AI.Labda umewahi kutumia AI bila hata kujua vizuri inavyofanya kazi. Unaweza kuitumia kutafsiri maneno, kuandika ujumbe,kutafuta mawazo, kujifunza jambo fulani,kufanya utafiti au hata kuandaa maudhui ya video na mitandao ya kijamii.Lakini pamoja na mambo yote hayo, kuna watu wengi ambao bado wana hofu kubwa kuhusu AI.

Baadhi wanauliza, “AI itatupeleka wapi?” Wengine wanaogopa kupoteza kazi zao.Wengine wanaona AI kama kitu ambacho kinaweza kuja kuwatawala wanadamu. Na kwa upande wa Wakristo, kuna maswali mengine ya kiimani: Je, AI ina uhusiano wowote na mambo ya mwisho wa dunia? Je, ni sahihi Mkristo kutumia AI? Je, teknolojia hii inaweza kuwa sehemu ya mpango wa Shetani?Haya ni maswali ambayo hayapaswi kubezwa. Ni maswali ambayo yanahitaji kujadiliwa kwa utulivu, maarifa na hekima.

Kwanza, AI ni nini?

Kwa lugha rahisi, AI ni teknolojia inayowezesha kompyuta kufanya baadhi ya kazi ambazo kwa kawaida tunazihusisha na uwezo wa mwanadamu.

Kwa mfano, AI inaweza kuchambua taarifa, kutafsiri lugha, kujibu maswali, kusaidia kuandika na kutambua mifumo mbalimbali.

Kwa mtu ambaye hajawahi kutumia teknolojia hii, inaweza kuonekana kama kompyuta imekuwa na akili kama ya mwanadamu.

Lakini ni muhimu kuelewa tofauti.

AI si mwanadamu.

Inaweza kuzungumza kwa namna inayofanana na mwanadamu, lakini hilo halimaanishi kwamba ni mwanadamu. Inaweza kutoa jibu zuri, lakini hilo halimaanishi kwamba ina dhamiri au maisha ya kiroho kama mwanadamu.

Na hapa ndipo tunapoanza kuelewa kwa nini elimu kuhusu AI ni muhimu.

Watu wanaogopa kile wasichokielewa

Mara nyingi mwanadamu huogopa kitu ambacho hakifahamu.

Ukimwambia mtu kwamba kuna mfumo unaoweza kuandika makala ndani ya sekunde chache, kutafsiri lugha na kujibu maswali mbalimbali, anaweza kujiuliza, “Hivi hii inaenda wapi?”

Ni swali la kawaida.Lakini badala ya kuogopa bila kuelewa, ni vizuri kujifunza.

Biblia inasema:“Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa.” Hosea 4:6

Mstari huu una mazingira yake ya kibiblia, lakini unatukumbusha umuhimu wa maarifa.

Hatuwezi kukabiliana na dunia inayobadilika kwa kufunga macho. Tunahitaji kujua kinachoendelea.

Kwa nini baadhi ya Wakristo wanaogopa AI?

Hili ni jambo la kuvutia.Mkristo anaweza kuiona AI na kujiuliza, “Hivi teknolojia hii ina uhusiano gani na imani yangu?”Wengine wanaweza kusikia kuhusu AI halafu mara moja wakaanza kuhusisha na Mpinga Kristo, alama ya mnyama au matukio ya siku za mwisho.Ni vizuri kuwa na tahadhari kuhusu mambo ya kiroho, lakini pia tunahitaji kuwa makini tusije tukaanza kusema Biblia imesema jambo fulani wakati Biblia haijasema hivyo moja kwa moja.

Si kila teknolojia mpya ni unabii wa Biblia.

Teknolojia ni chombo. Kinachotakiwa kuchunguzwa ni namna chombo hicho kinavyotumiwa na madhara au manufaa yanayoweza kutokea.

Je, kutumia AI ni dhambi?

Hili ni swali ambalo Wakristo wengi wanaweza kujiuliza.

Kwa mtazamo wangu,hatupaswi kuangalia jambo hili kwa kusema tu, “AI ni teknolojia, kwa hiyo ni dhambi,” au “AI ni teknolojia, kwa hiyo kila kitu kinachofanyika kupitia AI ni sawa.”Tunapaswa kuangalia matumizi yake.Simu inaweza kutumiwa kuhubiri Injili.Lakini simu hiyo hiyo inaweza kutumiwa kueneza mambo mabaya.Internet inaweza kutumiwa kujifunza Biblia.Lakini internet hiyo hiyo inaweza kutumiwa kwa mambo yasiyofaa.Pesa inaweza kutumiwa kumsaidia mtu mwenye shida, lakini inaweza pia kutumiwa kufanya uhalifu.Kwa hiyo, mara nyingi tatizo si chombo pekee, bali ni namna tunavyokitumia.Hivyo basi, Mkristo anapotumia AI anapaswa kujiuliza:

Ninaitumia kwa sababu gani?

·    Je, ninachofanya ni cha kweli?

·    Je, ninamdanganya mtu?

·    Je, ninatumia kazi ya mtu mwingine bila heshima?

·    Je, matumizi yangu ya AI yananisaidia au yananifanya niwe mvivu wa kufikiri?

Hayo ni maswali muhimu.

Hofu nyingine ni kupoteza kazi

Hii ni hofu ambayo hata mtu ambaye si Mkristo anaweza kuwa nayo.

AI inaweza kufanya kazi ambazo hapo zamani zilihitaji muda mwingi wa mwanadamu. Hilo linaweza kuwafanya watu waogope kwamba siku moja mashine zitachukua nafasi zao.

Hofu hii haipaswi kubezwa.

Teknolojia inapobadilika, baadhi ya kazi hubadilika pia. Lakini historia imetuonyesha kwamba mwanadamu amekuwa akibadilisha namna ya kufanya kazi kila mara teknolojia mpya inapokuja.

Kompyuta zilibadilisha ofisi.

Simu za kisasa zilibadilisha mawasiliano.

Internet ilibadilisha biashara.

Na sasa AI inaleta mabadiliko yake.

Kwa hiyo, badala ya kuuliza tu, “AI itachukua kazi yangu?” tunaweza pia kuuliza:

“Ni ujuzi gani ninaohitaji kujifunza katika kizazi hiki?”

Hapo ndipo tunapoanza kuiona AI si kwa hofu tu, bali pia kama changamoto ya kujifunza.

Tuesday, September 8, 2026

Checklist ya Usalama wa WhatsApp

 

Checklist ya Usalama wa WhatsApp

Tumia checklist hii:

·       Two-Step Verification imewashwa

·       Simu ina screen lock

·        Unajua Linked Devices zako

·        Hutoi verification code

·       Hutoi PIN

·        Hufungui links za ajabu

·        Hupakui apps zisizoaminika

·        Hukubali kila group

·       Huthibitisha maombi ya pesa

·       Hupuuzi updates

·        Unakagua Privacy Settings

·        Hushiriki taarifa nyeti bila sababu

·       Unajua namna ya kuripoti scam

·        Unajua namna ya kuondoa linked device usiyoijua

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (FAQ)

WhatsApp inaweza kuibiwa kwa verification code?

Verification code ni taarifa nyeti. Ukimpa mtu mwingine, unaweza kuweka akaunti yako katika hatari. Usimpe mtu code ambayo WhatsApp imekutumia.

Mtu akiniomba WhatsApp code nifanye nini?

Usimpe. Kama mtu anasema ametumiwa code kimakosa na anahitaji umtumie, kuwa makini. Huo ni ujanja unaotumiwa kwenye scams.

Two-Step Verification ya WhatsApp ni nini?

Ni kipengele cha ziada cha usalama kinachokuwezesha kuweka PIN ili kuongeza ulinzi wa akaunti yako.

Nifanye nini nikiona device nisiyoijua kwenye WhatsApp?

Kagua Linked Devices. Kama huitambui, unaweza kuiondoa kwenye akaunti yako na kuchukua hatua nyingine za usalama.

Je, WhatsApp scam inaweza kunipotezea pesa?

Ndiyo. Scammers wanaweza kutumia WhatsApp kukushawishi utume pesa au utoe taarifa zinazoweza kutumiwa katika udanganyifu.

Je, ni salama kubofya kila link ninayotumiwa WhatsApp?

Hapana. Kagua link na chanzo chake kwanza. Usibofye link inayotia shaka.

Kwa nini sipaswi kutumia WhatsApp iliyomodified?

Programu zisizo rasmi zinaweza kuongeza hatari za usalama na faragha. Ni salama zaidi kutumia programu rasmi kutoka chanzo kinachoaminika.

Je, ni salama kutumia WhatsApp kwenye computer?

Inaweza kuwa salama ukiwa unatumia kifaa unachokiamini na ukalinda akaunti yako. Ukifanya login kwenye computer ya mtu mwingine, hakikisha ume-log out na ukague Linked Devices.

Hitimisho: Usalama wa WhatsApp Unaanza na Wewe

WhatsApp inaweza kuwa chombo muhimu sana cha mawasiliano, biashara na kujenga mahusiano. Lakini kama ilivyo kwa huduma nyingine za mtandaoni, matumizi yake yanahitaji uangalifu.

1.   Usimpe mtu verification code.

2.   Usishiriki PIN yako.

3.   Usibofye kila link.

4.   Usiamini kila ujumbe.

5.   Usitume pesa kwa haraka.

6.   Usipuuze Linked Devices.

7.   Usipuuze Privacy Settings.

Usipakue programu zisizoaminika.Na muhimu zaidi, jifunze kutambua scams na phishing.Kumbuka kwamba scammers mara nyingi hawahitaji kuvunja mfumo wa teknolojia ili kupata kile wanachotaka. Wakati mwingine wanahitaji tu kumshawishi mtu awape taarifa mwenyewe.Kwa hiyo unapokuwa unatumia WhatsApp,tumia kanuni hii:

·       Fikiria kabla ya kubofya.

·       Thibitisha kabla ya kuamini.

·       Linda taarifa zako kabla ya kuzishiriki.

Usalama wako wa kidigitali ni jukumu lako.

Mbinu za Kujilinda Dhidi ya WhatsApp Scams

 

Mbinu za Kujilinda Dhidi ya WhatsApp Scams

Tumia kanuni hii rahisi:

STOP

S — Simama.
Usichukue hatua haraka.

T — Tafakari.
Jiulize kama ujumbe una mantiki.

O — Ondoa shaka.
Thibitisha taarifa kupitia chanzo kingine.

P — Protect.
Usitoe code,PIN,password au pesa bila uhakika.

WhatsApp kwa Biashara: Tahadhari Zaidi

Kama unatumia WhatsApp Business, usalama ni muhimu zaidi.Akaunti ya biashara inaweza kuwa na:

  • wateja;
  • contacts;
  • order information;
  • mawasiliano;
  • taarifa za bidhaa;
  • taarifa za malipo.

Mtu akipoteza udhibiti wa akaunti ya biashara, madhara yanaweza kuwa makubwa.Kwa hiyo wafanyabiashara wanapaswa kuwafundisha wafanyakazi wao kutambua phishing na scams. Wazazi Wanapaswa Kuwafundisha Watoto Nini Kuhusu WhatsApp?

Watoto wanapaswa kufundishwa:

  • kutowapa watu strangers taarifa binafsi;
  • kutobofya links zisizojulikana;
  • kutotuma picha binafsi kwa watu wasiowaamini;
  • kutokutana na mtu waliyejuana naye online bila usalama na ushirikishwaji wa mzazi/mlezi;
  • kuripoti ujumbe wa kutisha au wa ajabu;
  • na kutunza passwords na codes.

Elimu ya usalama wa mtandao inapaswa kuanza mapema.

WhatsApp na Privacy: Kwa Nini Ni Muhimu?

Privacy haimaanishi kuwa una kitu cha kuficha.Privacy ni uwezo wa kuamua:Nani anajua nini kuhusu wewe? Katika dunia ya kidigitali, taarifa zako zinaweza kuwa na thamani.Jina lako, namba yako,picha zako,contacts na taarifa zako nyingine zinapaswa kushughulikiwa kwa uangalifu.

Monday, September 7, 2026

Earn Money


 Earn money by click here

https://vnadexpress.com/register?ref=BA4168442

Je, WhatsApp Inaweza Kuhackiwa?

 

Je, WhatsApp Inaweza Kuhackiwa?

Neno “WhatsApp hacked” hutumiwa kwa maana tofauti.Wakati mwingine mtu anaweza kupoteza udhibiti wa akaunti baada ya kudanganywa na scammer.Katika hali nyingine,tatizo linaweza kuwa kwenye kifaa,akaunti iliyounganishwa,SIM au usalama wa mtumiaji.Ndiyo maana ni muhimu kuchunguza dalili na kuchukua hatua haraka.

Nifanye Nini Kama Nimepokea Verification Code Ambayo Sikuomba?

Kwanza, usiimpe mtu yeyote code hiyo.

Kama hukuomba verification code,inaweza kuwa mtu anajaribu kusajili namba yako au kuna jaribio fulani la kuingia au kuthibitisha akaunti.Kuwa makini na simu au ujumbe unaofuata unaokuomba code hiyo.Usishiriki code.

Nifanye Nini Kama Akaunti Yangu Inaonekana Kuwa Katika Hatari?

Hatua za msingi ni:

1.   Usimpe mtu verification code.

2.   Kagua Linked Devices.

3.   Ondoa vifaa usivyovitambua.

4.   Hakikisha Two-Step Verification imewashwa.

5.   Kagua privacy settings.

6.   Sasisha programu yako kutoka chanzo rasmi.

7.   Tumia njia rasmi za WhatsApp Help kama unahitaji msaada zaidi.

Usimpe mtu anayejitambulisha kama “support” taarifa zako za siri bila kuthibitisha kuwa ni njia rasmi.

Je,WhatsApp Messages Ni Salama?

WhatsApp hutumia end-to-end encryption kwa mawasiliano ya aina zinazoiunga mkono.Hii ina maana kwamba mawasiliano yanalindwa wakati yanasafirishwa kati ya watumiaji.Lakini mtumiaji bado ana wajibu wa kulinda:

  • simu yake;
  • verification code;
  • PIN;
  • backups;
  • linked devices;
  • taarifa anazoshiriki;
  • na maamuzi anayofanya mtandaoni.

Kwa maneno mengine:Encryption si ruhusa ya kuamini kila mtu.

Kwa Nini Scammers Hutumia WhatsApp?

WhatsApp ni maarufu katika nchi nyingi na watu huitumia kila siku.Hii huwafanya scammers kujaribu kuitumia kwa sababu wanaweza:

  • kuwasiliana moja kwa moja na mtu;
  • kujifanya rafiki;
  • kutuma links;
  • kutuma files;
  • kuunda groups;
  • kutumia social engineering;
  • na kushinikiza mtu afanye uamuzi haraka.

Ndiyo maana elimu ya cybersecurity ni muhimu.