Je, WhatsApp Inaweza Kuhackiwa?
Neno “WhatsApp hacked”
hutumiwa kwa maana tofauti.Wakati mwingine mtu anaweza kupoteza udhibiti wa
akaunti baada ya kudanganywa na scammer.Katika hali nyingine,tatizo linaweza
kuwa kwenye kifaa,akaunti iliyounganishwa,SIM au usalama wa mtumiaji.Ndiyo
maana ni muhimu kuchunguza dalili na kuchukua hatua haraka.
Nifanye Nini Kama Nimepokea Verification
Code Ambayo Sikuomba?
Kwanza, usiimpe mtu
yeyote code hiyo.
Kama hukuomba verification
code,inaweza kuwa mtu anajaribu kusajili namba yako au kuna jaribio fulani la
kuingia au kuthibitisha akaunti.Kuwa makini na simu au ujumbe unaofuata
unaokuomba code hiyo.Usishiriki code.
Nifanye Nini Kama Akaunti Yangu Inaonekana
Kuwa Katika Hatari?
Hatua za msingi ni:
1.
Usimpe mtu verification
code.
2.
Kagua Linked Devices.
3.
Ondoa vifaa
usivyovitambua.
4.
Hakikisha Two-Step
Verification imewashwa.
5.
Kagua privacy settings.
6.
Sasisha programu yako
kutoka chanzo rasmi.
7.
Tumia njia rasmi za
WhatsApp Help kama unahitaji msaada zaidi.
Usimpe mtu
anayejitambulisha kama “support” taarifa zako za siri bila kuthibitisha kuwa ni
njia rasmi.
Je,WhatsApp Messages Ni Salama?
WhatsApp hutumia end-to-end
encryption kwa mawasiliano ya aina zinazoiunga mkono.Hii ina maana kwamba
mawasiliano yanalindwa wakati yanasafirishwa kati ya watumiaji.Lakini mtumiaji
bado ana wajibu wa kulinda:
- simu yake;
- verification code;
- PIN;
- backups;
- linked devices;
- taarifa anazoshiriki;
- na maamuzi anayofanya mtandaoni.
Kwa maneno mengine:Encryption
si ruhusa ya kuamini kila mtu.
Kwa Nini Scammers Hutumia WhatsApp?
WhatsApp ni maarufu katika
nchi nyingi na watu huitumia kila siku.Hii huwafanya scammers kujaribu kuitumia
kwa sababu wanaweza:
- kuwasiliana moja kwa moja na mtu;
- kujifanya rafiki;
- kutuma links;
- kutuma files;
- kuunda groups;
- kutumia social engineering;
- na kushinikiza mtu afanye uamuzi haraka.
Ndiyo maana elimu ya
cybersecurity ni muhimu.
