22. Usimpe Mtu Simu Yako Iliyofunguliwa
Kama simu yako iko
unlocked, mtu anaweza kupata nafasi ya kuangalia taarifa nyingi.Hakikisha simu
yako ina:
- PIN;
- password;
- pattern;
- fingerprint;
- au njia nyingine ya screen lock inayopatikana kwenye
kifaa chako.Usalama wa WhatsApp haupaswi kuishia kwenye app pekee.Linda
simu nzima.
23. Usipuuze Privacy ya Status Yako
WhatsApp Status inaweza
kuonekana na watu kulingana na privacy settings zako.Kabla ya kuweka taarifa
binafsi kwenye Status, fikiria:Nani anaweza kuiona? Epuka kuweka taarifa
ambazo zinaweza kutumiwa vibaya, kama:
- eneo lako kwa wakati halisi;
- taarifa za safari;
- taarifa za fedha;
- nyaraka;
- taarifa za watoto;
- taarifa za familia;
- taarifa nyingine ambazo ungependa zibaki binafsi.
24. Usifikiri WhatsApp Inakuzuia Kila Aina
ya Scam
Hili ni jambo muhimu
kuelewa.WhatsApp inaweza kuwa na vipengele vya usalama, lakini scammer bado
anaweza kukutumia ujumbe wa udanganyifu.Kwa hiyo kuna tofauti kati ya:Security
ya mfumo na Usalama wa mtumiaji.Mfumo unaweza kukupa ulinzi, lakini
kama wewe mwenyewe utampa scammer verification code, PIN au pesa, teknolojia
pekee haiwezi kuzuia uamuzi huo.
25. Usipuuze Elimu ya Cybersecurity
Njia bora ya kujilinda si
kutumia technology tu.Ni kujifunza.
Jifunze kuhusu:
- phishing;
- social engineering;
- malware;
- identity theft;
- password security;
- two-factor authentication;
- privacy;
- scams;
- fake websites;
- online fraud.
Kadiri unavyojua mbinu
zinazotumiwa na scammers, ndivyo inavyokuwa rahisi kuzitambua.
No comments:
Post a Comment