13. Usifanye Forward ya Kila Ujumbe
Unaoupokea
WhatsApp inaweza kuwa njia
nzuri ya kusambaza habari.Lakini si kila habari unayopokea ni ya kweli.Kabla ya
ku-forward ujumbe, jiulize:Je, habari hii ni ya kweli?Angalia
chanzo.Ujumbe unaosema:
“WhatsApp imetangaza…”
“Serikali imesema…”
“Kesho kutakuwa na…”
“Benki imetoa…”
unapaswa kuthibitishwa
kupitia chanzo rasmi.Kusambaza taarifa za uongo kunaweza kusababisha hofu,
kuchanganyikiwa au madhara mengine.
14. Usihifadhi Taarifa Nyeti Kwenye Chat
Bila Sababu
Watu wengine hutumia
WhatsApp kama sehemu ya kuhifadhi:
- passwords;
- PIN;
- namba za kadi;
- taarifa za benki;
- nakala za nyaraka;
- taarifa nyingine nyeti.
Hii si tabia nzuri ya
usalama.Kama simu yako au akaunti yako itapata tatizo, taarifa hizo zinaweza
kuwa katika hatari.Tumia njia salama zaidi kuhifadhi taarifa nyeti.
No comments:
Post a Comment